Kuhusu Gustavsbergs IF HK
Karibu katika Kilabu Cha Mpira Wa Mikono Cha Gustavsberg (Gustavsbergs IF HK, ”GIF HK" ama "Gurra").
Gustavsbergs IF HK kimekuwepo Värmdö kwa zaidi ya miaka 30. Tuna jumla ya wachezaji-hai 400 wa mpira wa mikono (wavulana na wasichana, kati ya miaka 6 na miaka 19, pamoja na wachezaji wandamizi) na viongozi na wakufunzi wenye uzoefu mzuri na wanaojitolea sana.
Miongoni mwa viongozi na wakufunzi wetu 80 wa kujitolea na wasiolenga faida, wengi wao ni wazazi wa watoto wenye bidii michezoni, lakini pia tuna wakufunzi vijana.
Tunafanya mazoezi na kucheza mechi katika nyanja tofauti tofauti huku Värmdö, lakini mara nyingi huwa kwenye ukumbi wa Gustavsbergs Sporthall ulio karibu na kitovu cha Gustavsberg.
Sera yetu ya kilabu ni kuwa tunacheza mpira wa mikono ili kujifurahisha tu. Lengo ni kuwa wengi iwezekanavyo watataka kuucheza mpira wa mikono kwa muda mrefu iwezekanavyo, kisha baadaye maishani wafurahi kuendelea kama wakufunzi, makocha, marefa na kadhalika.
Tunatia bidii kuunda utamaduni wa ushiriki, uhusishaji, na kufurahia pamoja, sio tu kwenye timu bali hata kama kilabu - jumla ya kilabu inafaa kuwa zaidi ya vijisehemu binafsi, yaani timu.
Tunahudhuria kambi za pamoja za mazoezi na mashindano/vikombe na kila mara katika majira ya machipuko, siku yetu ya kilabu "Gurrabollen" ni dhihirisho kubwa la mpira wa mikono katika GIF HK.
Kadiri muda unavyopita, tumefanikiwa kushinda na pia kuwaelimisha wachezaji ambao wamefika timu zote mbili za kitaifa na wanacheza katika kiwango cha wachezaji bora. Lakini zaidi ya yote, tumeweza kupatia kila mtu anayependa mpira wa mikono biashara-wazi na yenye kuhusisha ambapo maadili-msingi yetu ni Furaha, Jamii, Maendeleo, na Mamboleo.
Ikiwa ungependa kujifunza zaidi na unataka kuujaribu mchezo huu bora wa mpira wa mikono, tafadhali wasiliana nasi kupitia Linda Olsson katika linda@gustavsberghandboll.nu au nambari ya simu 070 922 99 76.
Karibu katika Kilabu Cha Mpira Wa Mikono Cha Gustavsberg!!